Donate

Together We Can Provide Better Life to All Tanzanian Children

LOCAL FUNDRAISING

Construction of 

     LABOR WARD    

at Masanganya Dispensary in Kisarawe district

Short description:

Community Development Trust Fund of Tanzania (CDTF) collaborates with Masanganya village council to mobilize resources for the construction of labor ward. Masaganya is one of the villages in Kibuta ward, Kisarawe District Coastal region. The facility serves about 2,293 women aged between 15-49 years who are within the population catch up for women at Kibuta ward.

The expected result of the proposed project is to improve childbearing environment of more than 276 women per year expected to attend and get safe delivery and quality service.  At present there is only one room used for; labour service delivery, waiting room and Nurse Workplace, The space is small to accommodate all three activities mentioned above.

During Community Led Monitoring (CLM) activities, which is ongoing in the village, identified the challenge of labour ward as a priority case that need to be addressed immediately. Thus, CDTF and Masanganya community agreed to mobilize resources to construct a labor ward which will solve the present problem.

Donate through account below or contact us

Executive Director                                                                                                  Community Development Trust Fund (CDTF)                                                                    P.O. Box 9421, Dar Es Salaam                                                                                                Tel: +255 22- 2131472 +255784908140                                                                              E-mail: [email protected] or  [email protected]

  Maelezo Mafupi

Taasisiya Maendeleoya Jamii (CDTF) inashirikiana na halmashauri ya kijiji cha Masanganya kutafuta rasilimali kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi (Leba).

Masaganya ni moja ya kijiji  kwenye kata ya Kibuta Wilaya ya Kisarawe mkoa  wa Pwani. Zahanati ya Masanganya ambayo iko kata ya Kibutainahudumia wanawake wenye umri wa miaka 15-49 wenye uwezo wa kuzaa wapatao 2,293. . Takwimu kutoka zahanati ya Masanganya zinaonesha wajawazito 276 kila mwaka wanahudhuria kupata huduma za kujifungua kituoni.

Kwa sasa chumba ambacho kinatumika kutoa huduma za wazazi ni kidogo na hutumika kutoa huduma mchanganyiko za mzazi kujiandaa, kujifungua na ofisi ya wakunga. Aidha, chumba hicho kipo karibu na huduma zingine zinazotolewa kwa wagonjwa na hivyo kukosa usiri kwa wazazi wanaojifungua. Mara kadhaa imetokea wazazi wanapopata uchungu wa kujifungua na kuwepo na wagonjwa wengine wanaosubiri huduma kwenye jengo la zahanati wakunga huwaomba wagonjwa watoke nje ili kulinda heshima na utu wa mjamzito anayejifungua  asisikike na wagonjwa wengine. Kitendo hiki kwa upande mwingine kinasabisha usumbufu kwa wagonjwa waliofika kupata huduma.

Wakati wa utekelezaji na ufuatiliaji wa shughuli za (CLM) unaoendelea kwenye kijiji cha Masanaganya ambazo zinasimamiwa na CDTF kwa kufadhiliwa na PEPFAR, ilibainishwa kuwepo kwa changamoto ya kuwepo kwa chumba duni kinachotumika kama wodi ya  wazazi kujifungulia watoto suala hilo lilipewa  kipaumbele na jamii hivyo kuliwekea mpango wa utekelezaji .

Kufuatia uamuzi huo Halmashauri ya Kijiji Cha Masanganya imekubaliana na CDTF kushirikiana katika uhamasishaji wa kukusanya rasilimali ambazo zitasaidia ujenzi wa wodi ya wazazi kufikia Juni, 2022.

Ukiwa mdau wa Maendeleo unaombwa kuchangia kuwezesha ujenzi wa wodi ya wazazi Masanganya kwa kuwasiliana nasi au kutuma chochote kupitia mawasiliano ya hapo chini.

Bank name: NBC
Account Name: Community Development Trust Fund of Tanzania
Bank Branch: Azikiwe
Account number: 011103003058