Mwanafunzi Hamisi Nguku akipokea mahitaji kutoka CDTF yaliyowasilishwa na Mwalimu

CDTF inampongeza Hamisi Nguku kwa kufaulu mtihanmi wa kidato cha nne na kuchaguliwa kuendela na masomo yake ya kidato cha sita. Hamisi Nguku, kijana mwenye ulemavu anayetumia miguu kuandika kutoka kijiji cha Munga, kata ya Mtimbila, wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro.

CDTF imekuwa ikiwezesha vijana kupitia programu yake ya kusaidia wanafunzi kwa kutumia mapato ya ndani. Moja ya vijana waliowezeshwa ni Hamisi Nguku

Kwa zaidi ya miaka 20, CDTF imekuwa ikishirikiana na wafadhili mbalimbali, kama Operational Bootstrap Africa (OBA), kusaidia sekta ya elimu. Tangu mwaka 2020 CDTF imekuwa ikiwezesha vijana kupitia programu ya kusaidia wananfunzi kwa kutumia mapato ya ndani kuwapatia mahitaji ya shule kama vile madaftari, kalamu, sare za shule n.k.. Pia imekuwa ikiwawezesha nauli, kugharamia matibabu kwa wananfunzi wenye ulemavu wa ngozi.

Hamisi Nguku alipatikana kupitia taarifa zilizotolewa na mwalimu wake aliyesikiliza elimu ya maendeleo kutoka CDTF kupitia redio. Menejimenti ya CDTF ilifanya uchambuzi wa mahitaji ya Hamisi na kubaini kuwa anahitaji msaada ili aendelee na shule. Mnamo mwaka 2021, CDTF iliwasiliana na uongozi wa shule ya msingi Mtimbira na kumsaidia vifaa vya shule. Hata hivyo, ilibaini changamoto ya usafiri wa kumfikisha shule kwa urahisi, hivyo iliamua kumsaidia kupata kiti mwendo kutoka CCBRT.

Licha ya kupata kiti mwendo, miundombinu ya shule aliyosoma ilikuwa bado ni kikwazo. CDTF ilimhamishia shule ya msingi Kilosa, ambapo waliendelea kumpatia vifaa vya shule na nauli ya kwenda na kurudi nyumbani wakati wa likizo.

Hamisi alifaulu masomo yake ya sekondari kidato cha nne. CDTF ilijadiliana na mwalimu wake ili kuona namna ya kumhamishia kwenye shule yenye mazingira wezeshi kwa masomo ya sekondari. Ikiwa katika hatua hizo, serikali ilimsaidia kwa kumhamishia shule ya sekondari Kilosa alipokuwa anasomea kidato cha nne. Menejimenti ya CDTF inawashukuru wadau wote waliojitokeza kumsaidia Hamisi kufanikisha uhamisho wake na kuendelea na masomo.

CDTF inajivunia mafanikio haya na inaendelea kuhamasisha wadau kuchangia maendeleo ya Hamisi Nguku ili atimize ndoto zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *