Picha  ya pamoja ya baadhi ya vijana wakati wa  kukabidhiwa bajaji

Taasisi ya Maendeleo ya Jamii (CDTF) huwawezesha wananchi hususani vijana kushiriki katika shughuri za uchumi ili wajikwamue na umasikini uliokithiri. Mwanzoni mwa mwaka 2019 uongozi wa CDTF uliamua kuanzishwa kwa mfumo wa kuweka na kukopa (revolving fund) ili kuwajengea uwezo vijana kushiriki kwa vitendo katika kujikwamua kiuchumi. Mfumo huu kwa sasa unawezesha kuwakopesha vijana pikipiki za matairi matatu (bajaji) na kurejesha fedha za mkopo ndani ya miezi kumi na nane.

Kupitia mfumo huo, vijana sita (6) wa Manispaa ya Morogoro wamenufaika na mafunzo ya siku moja ya uendeshaji na usimamizi wa Bajaji pia kupatiwa pikipiki za matairi matatu (bajaji) pamoja na  kuelimnishwa changamoto zinazowakabili vijana katika kupata ajira ili wao kuwa chachu ya kuhamasisha wenzao kushiriki katika maendeleo .

Picha inaonyesha Fundi ramadhani akiwapa maelekezo ya matumizi ya bajaji na utunzaji ili kusaidia uendelevu

Ndugu Stanford Kalala afisa kutoka CDTF ambaye aliwakabidhi vijana hao Bajaji kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa CDTF aliwashauri vijana hao sita  kutumia  bajaji kwa uangalifu kwa kuwa bajaji hizo zinawapa ajira itakayowaingizia kipato na kuhudumia familia zao hivyo ni vyema kuzitunza na kuzifanyia service mara kwa mara. Aliendelea kusema vijana walipatiwa bajaji kuwa wana bahati ya kuwa jicho kwa wengine na kuwa endapo watafanya vema na kukabidhiwa hizo bajaji kuwa zao baada ya miezi kumi na nane watawezesha kutoa ajira kwa vijana wengine.. Aliongeza kuwa sekta ya usafiri wa bajaji inakua kwa kasi na akawapa rai kuwa ni jukumu lao kujiheshimu na kufanya kazi kwa uweledi ili kuigeuza kazi ya udereva wa bajaji kuwa kazi inayoheshimika.

 Ndugu Athumani Adelitho ambaye ni miongoni mwa vijana waliopatiwa babaji aliushukuru uongozi wa CDTF kwa wazo la kusaidia vijana na msaada waliotoa kwa vijana utakaowawezesha  kujikwamua na umasikini. Nukuu  “Naishurkuru CDTF kwa kuniwezesha kupata bajaji kuinua hali yangu ya kiuchumi, vijana tunapoona fursa kama hizi inabidi tujitokeze tupige umaskini vita”.

CDTF katika mpango huu inakusudia kusaidia vijana 20 kutoka Halmashauri tatu (3) za Tanzania ifikapo mwaka 2021 watakaokuwa wamejiajiri kupitia pikipiki za matairi matatu maarufu kama bajaji. .

Picha inaonyesha Fundi ramadhani akiwapa maelekezo ya matumizi ya bajaji na utunzaji ili kusaidia uendelevu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *