Jamii imehamasishwa kutambua watu wenye mahitaji maalumu Kwa kuwasaidia kuwapatia misaada mbalimbali Hasa ya kibinadamu.

Afisa Miradi Taasisi ya Maendeleo ya Jamii(CDTF) Stanford Kalala amesema hayo wakati wa kukabidhi vitu mbalimbali vilivyotolewa na taasisi hiyo kama msaada kwenye kituo cha Kilulu Community Rehabitation Centre kilichopo Temeke Pile Jijini Dar es Salaam kinachohudumia watoto wenye ulemavu mbalimbali kama vile viungo na watoto wenye mtindio wa ubongo.

“Sisi wenyewe inapaswa kuwa na uwezo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kama Watanzania kwa kuzingatia haya sisi kama CDTF tumetekeleza hili kwakuwa ni moja wapo ya Jukumu hasa kwenye kugusa maisha ya Wananchi wa hali ya chini kabisa, tumejipanga vyema kuhamasisha wadau mbalimbali kutenga asilimia moja ya faida iende kwenye masuala ya uhisani.”Alisema Stanford Kalala Afisa Miradi CDTF.

Stanford Kalala ameongeza Kwa kusema kuwa kama unapata mshahara au posho au fedha yako kwenye biashara basi sio mbaya kama tukiamua kutenga asilimia moja kwa ajili ya kuwasaidia wenye mahitaji na kwakutambua umuhimu huo Taasisi ya Maendeleo ya Jamii CDTF imeandaa mpango Maalumu wa kusaidia watu wenye mahitaji katika Jamii Kila ifikapo Mwisho wa Mwaka mwezi wa kumi na mbili ili kuadhimisha siku maalumu ya utoaji yaani Giving Tuesday ambapo Mwaka huu imempendeza Mungu kuadhimisha Kilulu Community Rehabitation Centre Temeke Dar es Salaam.

Kwa upande wake Jumma Rashid msimamizi Mkuu wa Kituo Cha Kilulu Community Rehabitation Centre ameshukuru uongozi mzima wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii CDTF Kwa kuwatembelea na kuwapelekea zawadi mbalimbali watoto lakini kikubwa zaidi ni kuwakumbuka watoto hao wenye ulemavu kuwapelekea vifaa maalumu vya kuwasaidia mazoezi, mikeka, magodoro na vitu vingine na hii imewapa faraja Kubwa wao kama wazazi wenye watoto wenye mahitaji Maalumu kuona kuwa Taasisi kama CDTF imewakumbuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *