Support People with Disabilities | Ushuhuda na ujumbe kwa walemavu
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii (CDTF) inashiriki katika kuboresha hali za watu wenye ulemavu ili wawe na uwezo kama watu wengine kuwajibika kiutamaduni, kiuchumi, kijamii na kisiasa, na kujitegemea.
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii (CDTF) ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na Lady Marion Chesham mwaka 1962 ikiwa na madhumuni ya kuwajengea uwezo wananchi kujitolea na kuwajibika katika shughuri za maendeleo kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ili kuondokana na umasikini.