Taasisi ya Maendeleo ya Jamii (CDTF) mwaka 2016/17 ilishirikiana na wananchi wa kijiji cha Maguruwe kata ya Bunduki Wilaya ya Mvomero kujenga madarasa matatu na ofisi ya Walimu shule ya msingi Maguruwe ili kuchochea na kuboresha sekta ya elimu .
Wanafunzi katika shule ya msingi Maguruwe walikuwa wakisomea katika madarasa yenye miundombinu isiyoridhisha kulinganisha na ubora unaotakiwa kwa shule za msingi nchini. Wanafunzi walisomea katika madarasa yasiyo na madawati ya kutosha, majengo ni ya muda mrefu yaliyojengwa kwa tope hivyo kuweka nyufa zilizohatarisha usalama wa wanafunzi na walimu wakati wakati wakitumia madarasa husika.
CDTF baada ya kupata maombi ya Halmashauri ya kijiji kuomba kusaidiwa kukamilisha madarasa mawili ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi yakisubili kuezekwa. CDTF baada ya kukaa na wanakijiji cha Maguruwe ilihamasisha wananchi kuchangia zaidi ili kujenga madarasa ili kuondokana na tatizo kuu la kuwepo kwa miundo mbinu mibovu. Baada ya jamii kupata barua ya kukubaliwa kusaidiwa ujenzi wa madarasa waliamua kuchangia nguvu zao ambazo ziliwezesha kukusanya mawe na kujenga msingi wa madarasa matatu na ofisi mchango wenye thamani ya takribani Tsh 12,915,000 CDTF imechangia Tsh 62,082,300. Jumla ya kuu Tsh 74,997,300 zilizotumika kugharamia ujenzi na kununua samani kwenye madarasa matatu na ofisi ya walimu. madarasa hayo matatu yalizinduliwa mwezi Februari, 2018 na Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo .
Katika Uzinduzi Mh Jafo alihamasisha wadau kujitokeza zaidi ili kuboresha miundo mbinu ya kujifunzia. Aidha kwa niaba ya Serikali Mh. Jafo aliahidi kutengwa kwa fedha za kujenga madarasa mengine yanayofanana na aliyoyazindua. Ahadi hiyo hivi sasa imetekelezwa kwa serikali kutoa fedha za ujenzi wa madarasa mawili ambayo yako hatua za ukamilishaji na matundu ya choo sita..
Akitoa ushuhuda Bwana Alex Ijani mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Maguruwe alielezea jinsi miundo mbinu ya majengo inavyosaidia wanafunzi kupata eneo bora rafiki la kujifunzia na walimu kufundishia i. Nukuu “Matarajio yetu kuwa wanafunzi wetu watafanya vizuri kwenye matokeo” . Aidha, ndugu. Abtensen Selemani Mkude Mwenyekiti wa kijiji cha Maguruwe ameishukuru taasisi ya CDTF kwa kusaidia rasilimari za kujenga madarasa ya kisasa ambayo yalizinduliwa na Waziri ambaye aliona umuhimu wa kusaidia madarasa zaidi, Nukuu “kufika kwa CDTF kijiji cha Maguruwe kumetoa mwanga na njia ya Serikali kuwezesha ujenzi wa madarasa mapya mawili na kukamilisha madarasa mawili ambayo yalikuwa hayajaezekwa ambayo yalijengwa na wananchi tokea mwaka 2015. kwa sasa shule ya msingi Maguruwe inayo madarasa bora na ya kutosha, Mwisho bwana Mkude alitoa wito kwa wazazi kuwahimiza na kuwasimamia watoto wao kusoma ili waweze kufaulu na kuendelea na elimu ya sekondari.