Viongozi wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii (CDTF) Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Henry Mgingi (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya CDTF Mhandisi Leon Msimbe (kulia) wakijadiliana jambo walipokuwa shule ya Msingi Mlimwa kushirikiana na viongozi wa serikali, wananchi na wadau mbalimbali kwenye uzinduzi wa bwalo la chakula na lengo likiwa ni kuhamasisha lishe mashuleni kwa wadau wa sekta ya elimu.
CDTF imekuwa ikishirikiana na Operation Boostrap Africa (OBA) kuboresha mazingira ya elimu nchini ikiwemo kujenga miundombinu ya madarasa na nyumba za walimu. Lakini uongozi wa CDTF kwa kushirikiana na wananchi uliamua kwa makusudi kuibua mradi wa kujega bwalo la chakula ili kuhamasisha wananchi, serikali na wadau mbalimbali kuangalia suala la lishe mashuleni.
CDTF ilishirikiana na KKKT, Manispaa ya Dodoma na wananchi kujenga bwalo la kisasa la chakula katika shule ya msingi Mlinwa, Dodoma kwa ufadhili wa Operation Boostrap Africa (OBA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *